De oorspronkelijke bijlage downloaden
TEKST MEENEEMFOLDER
Misheni yetu
Focus on Vision Foundation (FOV) inalenga kufanya kuona vizuri kupatikane kwa kila mtu kwa bei inayoweza kumudika. Sisi hujaribu kufikia hiyo kupitia usambazaji wa Focusspec: miwani maalum inayoweza kurekebishika. Inayoweza kurekebishika inamaanisha mtumiaji anaweza kurekebisha miwani hiyo kwa hitaji lake mwenyewe. Na anaweza kurekebisha nguvu ya miwani yake tena na tena.
Uwezekano mkubwa
Focusspec ina uwezo mkubwa wa kubadilisha maisha kuwa bora kwa sehemu kubwa ya idadi ya watu ulimwenguni. Sababu kuu ni kwamba kawaida hakuna wataalam wa macho na madaktari wa macho wa kutosha kwa watu bilioni 1 ambao hawapati matibabu wakati wanahitaji urekebishaji uchepukaji macho.
Yenye kumudika na inayopatikana kwa urahisi
Focusspec inatatua sehemu kubwa ya tatizo la uchepukaji macho kwa sababu watumiaji hawahitaji wataalam kuwarekebishia na kuwatengenezea miwani mpya. Watu wanaweza kurekebisha kwa urahisi nguvu ya miwani yao wenyewe. Focusspec pia inamudika na kwa maoni hayo ni suluhisho linalofaa kwa tatizo la ulimwengu wote: Gharama ya uzalishaji iko chini na FOV inawasilisha miwani kwa msingi usio wa faida kwa Mashiriki ya Kiserikali na Mashirika yasiyo ya Kiserikali.
Manufaa kwa watumiaji
Kwa watumiaji wa Focusspec kuna manufaa mengi:
(Pata) tena uwezo wa kuona na kusoma vizuri
Watoto walio na macho mbaya wanaweza kujiendeleza kupitia elimu hadi kiwango cha juu zaidi
Watu wanaweza kujitunza tena na kamwe hawatahitaji kutegemea watu wengine
Wakulima wanaweza kutofautisha mbegu kutoka kwa magugu
Watu wanaweza rekebisha vyombo vya mashine zao, nguo, viatu, na kadhalika
Boresha macho asante kwa miwani rahisi
Usambazaji na uuzaji wa kawaida wa
Focusspec inamaanisha chanzo kawaida cha mapato ya kudumu
Watu watafaidika zaidi kutoka kwa maisha yao!
Ndio tunaweza kusaidia!
Focusspec hutatua asimilia >90% ya matatizo yote ya uchepukaji macho ulimwenguni kote. Matatizo ya uchepukaji macho wa binadamu ni tatizo la ulimwengu wote ambalo linaathiri watu bilioni moja! Focusspec inapatikana katika modeli mbili. Modeli moja (presbyopia) ni kutoka +0,5 dpt hadi +4,5 dpt na modeli nyingine (myopia) ni kutoka -1 dpt hadi -5 dpt. Focusspec husaidia watoto na watu wazima. Asilimia 10% ya watoto wote wanaozaliwa watahitaji urekebishaji wa macho karibu na mwaka wao wa 10-15. Na mtu mzima yeyote atahitaji kiwango fulani cha urekebishaji wa macho anapozeeka. Focusspec inapatikana kwa bei inayomudika kwa mtu yeyote aliye na hitaji na itaboresha maisha yao mara moja.
Wasiliana nasi
Je, unataka kujua zaidi au kuagiza Focusspecs? Jisikie huru kuwasiliana nasi kwa habari zaidi.
[Adres e.d.]
ONYESHO LA TEKST
Lengo letu:
• kufanya urekebishaji wa macho kwa kila mtu anayeugua kutokana na matatizo ya uchepukaji macho na hana ufikiaji wa utunzaji wa macho au muundo msingi wa utaalam wa macho.
Njia yetu:
• ukuzaji, uzalishaji na usambazaji wa Focusspec
Kuzingatia mtumiaji:
• ( Pata)tena kuona
• Watoto wanaweza kukuza talanta zao kupitia elimu
• Watu wanaweza (pata)tena usaidizi wa kibinafsi
• Wakulima wanaweza kutofautisha mbegu kutoka kwa magugu
• Watu wanaweza kurekebisha vyombo vya mashine na vifaa, kushona nguo zao, viatu, na kadhalika
• Usambazaji wa kawaida wa Focusspec unamaanisha chanzo cha kawaida cha mapato ya kudumu
• Watu watafaidika zaidi kutoka kwa maisha yao!
Wordt vertaald, even geduld aub..
