3. UTAFITI WA SOKO
Soko limegawanyika katika sehemu kuu mbili.
Maziwa ghafi.
Uuzaji wa maziwa ghafi hautaruhusiwa kutokana na sababu za kiafya, ingawa sehemu kubwa ya biashara ya maziwa sasa hivi huendeshwa katika hali hiyo.
Maziwa yaliyosindikwa
Mbali na maziwa halisi (fresh) pia kuna soko la maziwa lala, Yoghurt, siagi, samli & jibini
MIKAKATI YA KUFIKIA MALENGO YASOKO
Kampuni inanuia kuuza maziwa yaliyosindiwa tu ambayo ni Maziwa yaliyochemshwa na kupoozwa,yoghurt ,Mtindi siagi ,samli & jibini. Kampuni haitauza maziwa ghafi,hii ni kutokana na kuzuiwa kisheria kwa afya ya walaji. Mikakati ya kampuni ni kuhakikisha inazalisha na kuuza bidhaa zinazokidhi viwango vya ubora. Hii imeonekana katika Mviwambo kwa miaka iliyopita wamekuwa wakizalisha bidhaa zilizo bora na zenye viwango vya juu.
MAHITAJI YA SOKO
Kuna ongezeko kubwa la uhitaji wa maziwa katika Wilaya ya Mbozi ,hasa mji wa Tunduma unaokua kwa kasi,pia Mkoa wa Mbeya kwa ujumla ikizingatiwa sasa mkoa una hadhi ya jiji.
Pia kumekuwa na uhitaji mkubwa wa maziwa yaliyosindikwa vijijini ambako mara nyingi hutumia maziwa ghafi kutoka kwa wafugaji wenzao.
MTAZAMO WA SOKO
Tunduma ni mji uliopo mpakani kati ya Zambia na Tanzania kwenye barabara kuu ya kimataifa itokayo Dar es salaam kwenda Zambia .Hali hii inafanya soko la kimataifa kwenye mji wa Tunduma likue haraka .
Inategemewa kuwa na uhitaji wa jumla wa bidhaa za maziwa ,Ulaji wa maziwa kwenye hotel na migahawa kuwa mkubwa pia.
Pia inategemewa kuongezeka uhitaji wa bidhaa za maziwa kwa nchi ya jirani Zambia ni mkubwa ikilinganishwa na uzalishaji wao.
Kampuni inategemea upanuzi wa uuzaji wa bidhaa za maziwa Zambia kupitia mpaka wa Tunduma.
Soko la siagi au samli ni dogo ikilinganishwa na bidhaa zingine. Kwa vile siagi au samli ni bidhaa yenye ubora mkubwa na hudumu kwa muda mrefu bila kuharibika , kampuni inategemea kusafirisha hadi masafa marefu kama vile kuuzwa Dar es salaam na Zambia.
UKUAJI WA SOKO
Mnamo mwaka 2006 uuzaji wa maziwa ulikuwa kwa 7.5% tangu mwaka 2001, hii ni kwa mujibu wa takwimu za Mviwambo .Makadirio yanaonesha kuwa miaka ijayo kutakuwa na ongezeko la 10% kwa mwaka
MGAWANYO WA MAUZO.
Bidhaa za maziwa zitauzwa kwenye maduka yote yaliyopo Vwawa na Tunduma ambapo Kampuni inategemea kununua mafriji na kuweka kwenye Mahoteli na kusambaza maziwa. Bidhaa zingine zitapelekwa kwenye maduka ya Supermarket ili kujitangaza zaidi na kufungua masoko.Vilevile Tunduma na Vwawa kutakuwa na wauzaji wa rejareja.Bidhaa zingine zitapelekwa vijijini ambako pia kuna uhitaji wa bidhaa za maziwa .Watakuwepo wauzaji wa jumla Vwawa.
MIPANGO YA MASOKO
Katika mwaka wa kwanza ,swala la masoko litatafsiriwa zaidi na Meneja na matokeo yake yanaweza kubadilishwa katika mpango wa biashara ili kuboresha zaidi.
WASHINDANI WAKUBWA
Washindani wakubwa kwenye soko ni wafugaji binafsi na wauzaji wa maziwa ghafi rejareja mitaani.Hata hivyo ushindani wao ni katika kukusanya na kuuza maziwaghafi.
4. UTEKELEZAJI WA MIKAKATI
4.1 BEI ZA BIDHAA
Wateja watategemea kupata bidhaa bora na uhakika wa bidhaa sokoni. Bidhaa zitauzwa kwa bei linganifu .Bei ya mauzo katika mpango wa biashara umezingatia wastani wa mauzo uliopo wilayani Mbozi .Unaweza kubadilika kutokana na mfumuko wa bei au kupanda kwa gharama za uzalishaji.
4.2 MKAKATI WA MAUZO
4.2.1 MTAZAMO WA MASOKO
Kampuni inategemea kuongezeka kwa mauzo kwa 10% kwa mwaka. Bei itategemea kuongezeka kwa 8% kutokana na mfumuko wa bei wa muda mrefu.
4.2.2 PROGRAMU YA MAUZO
Kutambulisha maziwa na bidhaa za maziwa kampuni imepanga kugawa sampuli za maziwa na bidhaa zitokanazo na maziwa bure katika Wilaya ya Mbozi kwa kutumia gari lenye vipaza sauti. Vipeperushi na Mabango na mbinu mbalimbali za matangazo vitatumika.
4.3 MATAZAMIO YA KAMPUNI (MILESTONES)
Kwa mwaka wa kwanza mauzo yatakuwa Tshs 880 milioni kwa lita 1,025,650. Kutakuwa na ongezeko la 10% za mauzo kwa mwaka.Uzalishaji utaongezeka kwa 10% kwa mwaka.
Mwaka 1 201 milioni 720,000 ltrs
Mwaka 2 202 milioni 792,000 ltrs
Mwaka 3 232 milioni 871,200 ltrs
Mwaka 4 265 milioni 958,320 ltrs
Mwaka 5 302 milioni 1,054,152 ltrs
5 TIMU YA UONGOZI
TAHADHARI YA HASARA
Biashara yoyote inayohusiana na kilimo zinawalakini kwa sababu zifuatazo:
• Uzalishaji unategemea hali ya hewa
• Uzalishaji wa mifugo unaweza kukumbwa na magonjwa ya mlipuko ambayo yanaweza kusababisha kusimama kwa biashara .
Kwa mfano ugonjwa wa miguu na midomo au ugonjwa wa Homa ya bonde la ufa.
• Mahitaji ya bidhaa hubadilika kwa kuwa Tanzania inaendesha uchumi wa soko Huria , hivyo kuna uingizaji wa bidhaa za maziwa kutoka nje ya nchi kama vile maziwa ya unga n.k.
• Jinsi kampuni inavyozidi kuwa kubwa ndivyo mikopo inavyohitajika katika uendeshaji wake.
Kutokana na hizo tahadhari za hasara ambavyo kampuni inaweza kupata ,hivyo kampuni inategemea mambo yafuayayo;
• Uchumi wa Tanzanzania utaendelea kukua
• Watumiaji wa biadhaa zitokanazo na maziwa ndani ya nchi na nchi karibu ya Zambia wataongezeka kutokana na mabadiliko ya uhitaji wa vyakula.
• Baadhi ya maeneo ya Tanzania kuna uzoefu wa ufugaji wa Ng’ombe wa maziwa kama vile Wilaya ya Mbozi.
• Hali ya hewa ya Mbozi ni ya ubaridi hivyo kuruhusu ufugaji wa Ng’ombe wa maziwa.
• Mwisho ,matokeo ya kampuni yanategemea kuwa imara zaidi ikilinganishwa na uzalishaji .Bei kubwa ya maziwa ghafi itasababisha bei ya bidhaa za maziwa kuwa kubwa na kinyume chake.
5. HITIMISHO
Mpango wa biashara wa Mviwambo na Misingi ya wafugaji ni halisi, imejikita katika uzoefu wa miaka mingi katika ufugaji nchini Tanzania na Uholanzi na umeonesha matokeo chanya hata katika miaka miwili ya mwanzo .Hivyo huu ni mpango endelevu.
KAMPUNI YA KUSINDIKA MAZIWA MBOZI (MBOZI MAZIWA LIMITED)
1. Wastani wa uzalishaji kwa kila kikundi kwa siku (Production coefficients)
Jina la kikundi Kiwango cha maziwa kwa lita
Vwawa 500
Ndolezi 140
Hasamba 100
Hanseketwa 300
Mahenje 300
Mlowo 300
Isangu 200
Mbozi Mission 160
Total 2000
Losses (Promotion 15% ) 300
Halisi 1700
2. Uzalishaji wa maziwa kwa mwaka kila kiundi pamoja na ongezeko la 10% kwa mwaka, kiwango ni kwa lita
Jina la kikundi Mwaka 1 Mwaka 2 Mwaka 3 Mwaka 4 Mwaka4
Vwawa 180,000 198,000 217,800 239,580 263,538
Ndolezi 50,000 55,000 60,984 67,082 73,791
Hasamba 36,000 39,000 43,560 47,916 52,708
Hanseketwa 108,000 118,800 130,680 143,748 158,123
Mahenje 108,000 118,800 130,680 143,748 158,123
Mlowo 108,000 118,800 130,680 143,748 158,123
Isangu 72,000 79,200 87,120 95,832 105,415
Mbozi Mission 57,000 63,360 69,696 76,666 84,332
Jumla 720,000 792,000 871,200 958,320 1,054,152
3. Mgawanyo wa maziwa kutokana na bidhaa zitakazozalishwa kwa mwaka
Jina la bidhaa Mwaka 1 Mwaka 2 Mwaka 3 Mwaka 4 Mwaka 5
Fresh milk 360,000 396,000 435,600 479,160 527,076
Sour milk/Mtindi 144,000 158,400 174,240 191,664 210,830
Yoghurt 208,800 229,680 252,648 27,7913 305,704
Siagi/Butter 72,00 7,920 8,712 9,583 10,542
Jumla 720,000 792,000 871,200 958,320 1,054,152
4. Mgawanyo wa uzalishaji wa bidhaa kwa siku na bei ya maziwa (650/L)
Jina la bidhaa Asilimia za Bidhaa Kiwango halisi Bei /L Gharama za siku
Fresh milk 50 1000 650 650,000
Sour milk/Mtindi +/-20 400 650 260,000
Yoghurt +/-29 580 650 377,000
Siagi/Butter 1 20 650 13,000
100 2000 1,300,000
5. Gharama za ununuzi wa maziwa kwa kila lita ya maziwa (Tshs 650/lita) pamoja na mfumuko wa bei 8%.
Jina la kikundi Mwaka 1 Mwaka 2 Mwaka 3 Mwaka 4 Mwaka 5
Vwawa 117,000,000 138,996,000 152,895,600 168,185,160 185,003,676
Ndolezi 32,760,000 38,918,800 42,810,768 47,091,564 51,801,282
Hasamba 23,400,000 27,799,200 30,579,120 33,637,032 37,001,016
Hanseketwa 70,200,000 83,397,200 91,737,360 100,911,096 111,002,346
Mahenje 70,200,000 83,397,600 91,737,360 100,911,096 111,002,346
Mlowo 70,200,000 83,397,600 91,737,360 100,911,096 111,002,346
Isangu 46,800,000 55,598,400 61,158,240 67,274,064 74,001,330
Mbozi Mission 37,440,000 44,478,720 48,926,592 53,819,532 59,201,064
Jumla 468,000,000 555,983,920 611,582,400 672,740,640 740,015,406
6. Gharama za ununuzi wa maziwa kwa uwiano wa bidhaa zitakazozalishwa na kiwanda
Jina la bidhaa Mwaka 1 Mwaka 2 Mwaka 3 Mwaka 4 Mwaka 5
Fresh milk 234,000,000 277,992,000 305,791,200 311,454,000 342,599,400
Sour milk/Mtindi 93,000,000 102,960,000 113,256,000 124,581,600 137,039,500
Yoghurt 135,720,000 149,292,000 164,221,200 180,643,450 198,707,600
Butter/Siagi 4,680,000 5,148,000 5,662,800 6,228,950 6,852,300
Jumla 468,000,000 535,392,000 588,931,200 622,908,000 685,198,800
7. Mauzo ya maziwa kwa uwiano wa mgawanyo kwa asimilia
Jina la bidhaa Asilimia Kiwango kwa lita Bei/L Mauzo kwa lita
Fresh milk 50 850 1,400 1,190,000
Sour milk/Mtindi +/-20 340 2,000 680,000
Yoghurt +/-29 493 2,400 1,183,200
Butter/Siagi 1 17 3,000 51,000
Jumla 100 1,700 3,104,200
8. Mauzo ya maziwa na bidhaa zake kwa mwaka pamoja na ongezeko la 10%
Jina la bidhaa Mwaka 1 Mwaka 2 Mwaka 3 Mwaka 4 Mwaka 5
Fresh milk 428,400,000 471,240,000 518,364,000 570,200,400 627,220,440
Sour milk/Mtindi 244,800,000 269,280,000 296,208,000 325,828,800 358,411,680
Yoghurt 425,952,000 468,547,200 515,401,920 566,942,112 623,636,323
Butter/Siagi 18,360,000 20,196,000 22,215,600 24,437,160 26,880,876
Jumla 1,117,512,000 1,229,263,200 1,352,189,520 1,487,408